Menu
 

 Bwana Elia Daudi Mwalonde mkazi wa Uyole akiwa hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya wodi namba 1 baada ya kupigwa nondo.
 Bwana Meshack Kombo Mwakibinga mwenye umri wa miaka 33, mzaki wa Chunya alipingwa nondo eneo la Soweto jijini Mbeya akiwa hospitali ya Rufaa Mbeya wodi namba 1.
Bwana Zefania Mwangwale mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa Uyole akiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya. Tukio hili lilimkuta Bwana Zefania akiwa na wenzake Hans Kyando na Shitambali Shitindi wakiwa kwenye Grocery ya WP Frola walivamiwa na kupingwa nondo na kuporwa simu aina ya Nokia na Pesa taslmu shilingi 420,000/= mali ya Askali WP FROLA ambaye ni mmiliki wa Grocery hiyo.iliyopo Uyole jijini Mbeya.

Wito umetolewa kwa wananchi kujitolea damu kwa ajiji ya kuwanusuru wahanga wa janga la kupingwa nondo ambao katika Wodi namba 1 mtandao huu umebaini kuwepo kwa zaidi ya majeruhi 9.

Picha na habari kwa ushirikiano wa Kamanga na MatukioMbeya Yetu na Chimbuko Letu.

Post a Comment

 
Top