Menu
 

  Kulia ni Capt.Sambwee Shitambala akiwa na mmiliki wa blog hii Gordon Kalulunga katika viwanja vya Uyole ya kati wakati wa Fainali ya Edi Cup iliyohitimishwa jana.
  Wachezaji wa timu ya Edi Sekondari wakimsikiliza kocha wao.
 Mashabiki kadhaa wakiendelea kuangalia mtanange wa fainali ya Edi Cup kati ya timu ya Edi Sekondari na Mponja Sekondari. Kulia ni George Mwaikela na mwanae wa kiume.
  Wachezaji wa Timu ya Edi Sekondari ambao ni washindi wa ligi hiyo wakishangilia baada ya kuisha kwa ligi hiyo huku wakisubiri kukabidhiwa zawadi zao.
 Waamuzi wa fainali hiyo wakiwa wanajadiliana jambo na meza kuu ya uratibu wa ligi hiyo katika viwanja hivyo.
Wachezaji wa timu ya Mponja Sekondari wakimsikiliza Mwalimu wao ambaye aliwaamuru watoke uwanjani na kususia mchezo wa fainali hiyo.
TIMU maalum ya vijana wenye vipaji vya soka mkoani Mbeya imechaguliwa katika mashindano ya ligi kuu ya Edi Cup iliyomalizika jana Jijini Mbeya.

Vijana hao kutoka shule 16 za Sekondari zilizoshiriki katika mashindano hayo watalelewa na ofisi ya sheria ya Shitambala Advocates yenye makao yake makuu Jijini Mbeya.

Kuchaguliwa kwa timu hiyo kumetokana na Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Sheria Capt. Sambwee Shitambala kuvutiwa na vipaji vya vijana hao ambao alisema kuwa atawalea kwa kuwapatia vifaa vya michezo na mahitaji mengine ya kimichezo.

Wakati wa kufunga ligi hiyo, Capt. Shitambala alisema alifurahishwa na michezo hiyo ambayo ilianza kutimua vumbi Agosti 6 mwaka huu na kwamba timu hiyo iliyoundwa anaamini itatoa changamoto ya soka ndani ya nchi na nje ya nchi.

''Timu hiyo ya vijana 20 nitailea mimi na kuhakikisha inatoa changamoto ya soka nchini na nje ya nchi na wachezaji hao watauzwa katika vilabu mbalimbali zikiwemo timu za Simba na Yanga'' alisema Shitambala.

Sanjari na hayo alionya walimu wa michezo kuwa wanapaswa kuwa kioo cha nidhamu kwenye michezo badala ya kuwashawishi wachezaji kutoka nje ya uwanja pindi zinapojitokeza dosari za kiuamuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Edi SekondariGodfrey Mwatujobe ambaye alikuwa ni mwandaaji wa mashindano hayo kwa kushirikiana na Shitambala Advocate alisema michezo hiyo imewaletea faraja kubwa wanafunzi na jamii iliyokuwa inajitokeza katika viwanja hivyo kushuhudia vipaji vya wachezaji.

Timu zilizoshinda katika ligi hiyo na kupewa zawadi ni pamoja na timu ya Edi Sekondary iliyoshika nafasi ya kwanza na kupata zawadi ya jezi pea moja, mipira miwili na fedha taslimu Tsh.20,000/=, Mponja Sekondary jezi pea moja, mpira mmoja na Tsh.20,000/=.

Zingine ni Pankumbi Sekondari na Ilomba Sekondari huku mwalimu aliyeonesha ushirikiano katika michezo hiyo akipatiwa zawadi kutoka Pankumbi Sekondari na mchezaji Bora Rogers Kamage akitoka Edi Sekondari na Golikipa bora akitoka Ilomba Sekondari.

Post a Comment

 
Top