Menu
 

Na mwandishi wetu.
Wafanyabiashara wa soko la Nonde lililopo kata ya Itiji jijini Mbeya wameiomba halmashauri ya jiji kuwaboreshea miundombinu ya soko hilo ikiwa ni pamoja na kuwajengea dampo la kuhifadhia taka.

Wakiongea kwa nyakati tofauti tofauti wafanyabishara hao wamesema kuwa vyoo vinavyotumika kwenye soko hilo vimeharibika na havina mabomba ya kupitisha maji safi.

Mmoja wa wafanyabiashara hao Joshua Mwaipole amesema pamoja na kulipa ushuru wa shilingi mia mbili kila siku lakini hawaoni jitihada zozote za uongozi wa halmashauri ya jiji katika kuboresha miundombinu ya soko hilo.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Itiji Leonard Magoma amekanusha malalamiko yanayotolewa na wafanyabiashara hao kutokana na soko hilo kufanyiwa usafi kila siku.

Post a Comment

 
Top