Menu
 

Abbas Kadoro Mkuu mpya wa mkoa wa Mbeya aliyeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete juzi akila kiapo mbele ya Rais wakati wakuu wa mikoa mbalimbali walipoapishwa Ikulu leo jijini Dar es salaam(Picha kwa hisani ya FULL SHANGWE)
+++++
 Na mwandishi wetu.
Wafanyabiashara katika Soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya wamemlalamikia Mkuu wa mkoa kufuatia kauli yake yakusitisha ujenzi wa vidbanda vya matofali sokoni hapo nakuwataka kujenga vibanda vya mbao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii kwaniaba ya wafanyabiashara wenzake Bwana Anyandwile Mwalwiba amesema wanasikitishwa na kaulihiyo huku wakimuomba mkuu wa mkoa huyo kuwaruhusu kafanya ujenzi wa matofali japo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Bwana Abbas Kandoro amezua utata na mjadala kwa wafanyabiashara wa soko hilo wakati alipotembelea soko hilo huku uongozi wa halmashauri ya jiji ukibaki kimyabila kutoa utetezi kwa wafanyabiashara waliounguliwa na vibanda vyao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa soko hilo Bwana Charles Syonga amesema kuwa wafanyabiashara na viongozi wanapaswa kufuata agizo la mkuu wa mkoa, ukizingatia eneo hilo sio rasmi na mkataba wa halmashauri na Sido umeshakwisha..

Post a Comment

 
Top