Menu
 

Na mwandishi wetu.
Afisa kilimo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Dickson Maruchu amesema kuwa wasambazaji ambao watabainika kuuza pembejeo za kilimo feki watatozwa faini ya shilingi milioni kumi pamoja na kifungo cha miaka mitatu jela.

Ametoa onyo hilo wakati akifungua mafunzo ya siku sita ya mawakala wa pembejeo za kilimo na mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa pembejeo.

Naye mmoja wa wakulima wilayani humo Hamad Shaban amesema moja ya vitu vilivyochangia wakulima kupata mavuno hafifu mwaka huu ni kutumia mbegu na mbolea zilizopita muda wake.

Kwa upande wake mshauri wa shirikisho la mpunga wilayani Mbarali Bi.Anna Mkenga ameiomba serikali kufuatilia kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na kuchukuwa hatua kali dhidi ya mawakala wanaouza pembejeo za kilimo feki ili kuwanusuru wakulima dhidi ya umasikini.

Post a Comment

 
Top