Menu
 

Na mwandishi wetu.
Wafanyabishara wa eneo la Mwambene kata ya Ilomba jijini Mbeya wameiomba serikali kuwatengea eneo maalum kwa ajili ya soko kutokana na eneo wanalouzia kwa sasa kutokuwa rasmi.

Akiongea na mwandishi wetu mmoja wa wakazi wa eneo hilo bwana Simoni Nyika amesema kuwa anakerwa na kitendo cha wafanyabiashara hao kuuza bidhaa zao katika eneo la barabara kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao.

Naye mmoja wa wafanyabiashara hao Bi Grace Kisonga amesema kuwa kipindi cha nyuma walitakiwa kuhama na kwenda eneo lililopo mbali kidogo na barabara hiyo lakini imeshindikana kwani eneo hilo linamilikiwa na mtu binafsi.

Ameongeza kuwa kutokana kushindwa kulipia eneo hilo imepelekea wafanyabiashara hao kuendelea kuuza bidhaa kwenye eneo hilo la barabara.

Post a Comment

 
Top