Menu
 

Na mwandishi wetu.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana John Livingstone Mwakipesile ametoa msaada wa fedha shilingi laki tano kwa kikundi cha wajane kilichopo kijiji cha Mbebe, wilaya ya Ileje kwa ajili ya kujikimu na kutetea hakizao ndani ya jamii.

Amesema lengo la msaada huo ni kutetea haki za wajane kutokana na hali ngumu wanayokabiliwa kutokana na kunyang’anywa mali zao baada ya kufiwa na waume zao.

Bwana Mwakipesile ameyataka mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali kuwaangalia wajane na kuwapatia misaada ili kuondokana na dhana potofu ya kutengwa katika jamii inayowazunguka.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi.Nuru Msokwa amesema kuna wajane 24 ambao kwa sasa wamezalisha shilingi milioni moja na fedha hizo zimewasaiduia kuanzisha miradi ya maendeleo kwakuwakopesha wajane hao na kulipa kwa riba ndogo ndogo.

Pia amemshukuru mkuu wa mkoa kwa kuwapatia msaada huo na kuutumia kwa lengo lililokusudiwa na amewaomba viongozi wengine wa serikali kuiga mfano wa Mkuu huyo wa mkoa kwa kuwasaidia wajane kuondokana na umasikini.

Post a Comment

 
Top