Menu
 

Mganga mkuu    wa  mkoa  wa Mbeya   Dakta  Seif Mhina  ametoa onyo dhidi ya wamiliki wa maduka ya kuuzia dawa za binadamu na vituo vidogo vya afya kulaza wagonjwa na badala yake amewataka kuwafikisha wagonjwa wenye hali mbaya hospitali ili waweze kupatiwa matibabu sahihi.

Amesema   hayo wakati akitoa ufafanuzi wa sheria mpya ya huduma ya afya kwa binadamu katika semina ya siku moja kwa wamiliki wa vituo vidogo vya afya na wenye maduka ya kuuzia dawa.

Awali mganga mkuu wa jiji la Mbeya Dakta Samwel Lazaro amesema kuwa Ofisi yake imeanzisha ukaguzi maalumu kwa vituo hivyo vya afya jijini hapa ili kudhibiti matumizi ya vituo vidogo vya afya kulaza wagonjwa.

Post a Comment

 
Top