Menu
 

Licha ya mamlaka ya viwanja vya ndege mkoa wa Mbeya kutoa Onyo dhidi ya wananchi waishio pembezoni mwa uwanja wa ndege Mbeya la kuwataka kutokatisha uwanjani bado wamekuwa wakikaidi amri hiyo kwa kukatisha uwanjani mara kwa mara.

Pamoja na onyo kutolewa pia mamlaka hiyo imechimba mashimo na kujenga kuta ili kuzuia wananchi kukakatisha lakini bado wananchi hao wamekuwa wakidondosha kuta hizo pamoja na nyaya zilizowekwa ili waweze kukatisha kwa urahisi.

Uwanja wa Ndege Mbeya umekuwa ukitumiwa kama njia mbadala ya wakazi wa Air Port, Iyela, Hali ya Hewa na Maendeleo kukatisha kwenda kufuata mahitaji mbalimbali katikati ya jiji.

Hata hivyo wakazi hao wamekuwa wakitumia usafiri mwingine wa moto kama magari na pikipiki kukatisha uwanjani hapo hali inayohatarisha usalama wa usafiri wa anga wakati wa kutua au kuruka.

Awali mkuu wa kitengo cha ulinzi uwanjani hapo Bwana Peter Mbunghi alisema kuwa mwananchi atakayekamatwa akikatisha uwanjani hapo atatozwa faini ya shilingi elfu 30 hadi hamsini ikiwa ni adhabu kwa kukatisha uwanjani hapo.

Post a Comment

 
Top