Menu
 

Na mwandishi wetu.
Wananchi wa kijiji cha Inyala katika Halmashauri ya Mbeya Vijijini wameiomba radhi serikali kufuatia vurugu zilizo ibuka agost 28 mwaka huu kwa kutaka kuichoma moto kituo kidogo cha polisi na kupanga mawe barabarani kwa lengo la kushinikiza wenzo Wawili waliokamatwa kuachiwa huru kituoni hapo kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya mtu mmoja ambaye anasadikwa kuwa ni mwizi.

Akitoa maelezo mafupi leo mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo ndugu Evansi Balama katika kikao cha dharura kwa niaba ya Wananchi hao Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Ndugu Yusufu Abdala amesema kufuatia vurugu hizo wameiomba serikali iwasamehe kutokana na kutofahamu taratibu na sheria zinazo kataza kufanya maandamao bila kufuata taratibu na sheria zilizopo.

Amesema mara baada ya wakazi wa kijiji hicho kukivamia na kuanza kukishambulia kituo cha polisi kilichopo kijijini hapo kwa kupinga kitendo kukamatwa wenzao wawili waliojeruhiwa kwa kuchomwa kisu na kupigwa nondo na mtu mmoja anayesadikiwa kuwa mwizi ambaye baadaye aliuwawa na wanakijiji hao ni kutokana na kukusanyika kwa makundi mbalimbali yenye hisia tofauti.

Amesema kitendo cha mtu huyo kuvamia kijijini hapo nakuvunja duka la mfanyabiashara mmoja kijijini hapo na kupora vitu kaadha ndiko kuliko sbabisha wananchi hao kupandwa na hasira na kuanza kumfukuza kisha na kunza kumpiga hadi kusababisha kifo chake

Akijibu taarifa hiyo Mkuu huyo wa Wilaya Mbeya amesema kuwa kitendo cha kutokea kwa vurugu hizo nikuitia aibu kubwa serikali kutokana na eneo hilo kuwa kiungo kikubwa cha kupitisha malighafi kwenda nchi jirani za kusini mwa Afrika.

Amesema yeye kwa upande wake alitegemea wanachi wa eneo hilo wangekuwa na hali nzuri ya maisha kutokana na fursa zilizopo hasa katika sekta ya barabara na muindo mbinu ilyopo hivyo haoni sababu ya wao kuanzisha vurugu hizo na kutaka kuhalibu miundo mbinu hiyo ilihali bado ni masikini.

Amesema katika vurugu hizo idadai kubwa ya wananchi wamekuwa wakifuata mkumbo bila kujari madhra yanayo weza kutokea baadaye hivyo suala hilo halitaweza kuvumilika hata kidogo kweni watu wao wamepaka serikali matope.

Aidha Balama amesema Kwa yeyote aliyehusika katika vurugu hizo atashughulikiwa mara baada ya upelelezi kukamilika kweni vitendo hivyo vimekuwa vikijitokeza marakwa mara kutokana na wnanchi kutumia Uhuru uliopo vibaya kwa kujisahau bila kufuta taratibu nasheriaz zilizopo.

Pia Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito kwa wananchi hao kutokubali kushawishika na mtu yoyote kwa elimu yake au uongozi alionao kwa masilahi yake binafsi bila kujari utu wa mtu kwani kunaweza kusababisha maafa makubwa kwa wananchgi hao.

Vurugu hizo zilitokea Miwishomi mwa mwezi agosti kutokna nawananchi hao kupinga hatua ya serikili kuwakamata wenzo wawili kwa madai ya kuhusikka katika mauii ya mtu mmoja aliyesadikuwa kuwa ni mwizi kitendo kilicho wafayanya askari wa kutuliza ghasia kuwatawanya wananchi hao kwa mabomu ya machozi . (Kwa hisani ya Pastor Kalulunga na Tanzania yetu) 

Post a Comment

 
Top