Menu
 

 Hili ni Eneo la Mafiati jijini Mbeya.
Na mwandishi wetu. 
Waosha magari eneo la Mafiati jijini Mbeya wametakiwa kuhama katika eneo hilo kutokana na uchafuzi wa mazingira wanaoufanya ambao umekuwa ukihatarisha afya kwa wakazi wa eneo hilo.

Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Bwana Juma Iddi amesema uamuzi wa kuhamisha kwenye eneo hilo imetokana na hpofu ya kuibuka kwa magonjwa ya mripuko ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa mazingira.

Nao baadhi ya waosha magari hao wamekiri kutumia eneo hilo bila utaratibu maalumu ikiwa ni pamoja na kutokuwa na kibali cha kutumia eneo hilo.

Post a Comment

 
Top