Menu
 

Na mwandishi wetu
Ushirika wa Yerusalem Air Port jijini Mbeya wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi kupitia Umoja wa Wanawake umetoa msaada wa fedha, mavazi na vifaa kwa watoto 11 waishio katika mazingira magumu katika kituo cha Mbozi Misheni/mission kilichopo Mbozi mkoani hapa.

Akizungumza na mwandishi wetu Mchungaji Paul Mwambalaswa aliyekabidhi msaada  kwa niaba ya umoja huo amesema wametoa sabuni sukari nguo na fedha taslimu shilingi 135000 na kwamba wataendelea kutoa misaada katika vituo mbalimbali kadri watakavyoweza.

Aidha Mwenyekiti wa  Umoja huo Bi.Edda Kapola pamoja na Mchungaji Mwambalaswa wametoa wito kwa msaada huo kutumika ilivyokusudiwa  na pia wanajamii wajenge mazoea ya kuwasaidia wahitaji kwani MUNGU huwabariki wanaowasaidia wahitaji.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya watoto Makamu Mwenyekiti wa kituo hicho Bi.Rehema Mtambo ameupongeza umoja wa kinamama na kanisa kwa ujumla kwa kuwathamini na kuwatunza kiroho na kimwili na ameiomba jamii kuwa bega kwa bega  katika kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu ili wawe na maisha bora.

Post a Comment

 
Top