Menu
 

Na mwandishi wetu.
Waumini wa kanisa la waadventista wa sabato wameshauriwa kuishi maisha ya kiroho na yatakayoleta mafanikio katika maisha yao na Taifa kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa na katibu wa kanisa la waadventista Bwana Elias Romai hivi karibuni katika mahafali ya shule ya msingi Maps inayomilikiwa na kanisa hilo liliopo kata ya Iganzo jijini Mbeya.

Amesema kuwa licha ya mafunzo ya vitendo yanayotolewa kwa wanafunzi shuleni hapo bado kuna haja ya wazazi na wanafunzi kushiriki kwenye ibada na maombi ili kuiomba shule na Taifa katika maendeleo kwa ujumla.

Post a Comment

 
Top