Menu
 

 Watoto wadogo kabisa  wakitumikishwa katika upondaji zege/kokoto.
+++++
Na mwandishi wetu.
Wazazi jijini Mbeya wameshauriwa kuwapeleka watoto shule shule kwa lengo la kunufaika na elimu na badala yake kuepukana na makundi yasiyofaa ndani ya jamii yakiwemo ya wizi, kucheza kamali, kutumiwa kuuza madawa ya kulevya na bidhaa za wizi na ajira za utotoni.. 

Hayoyamesemwa na Mwenyekiti wa shirika la haki za Binadamu lililopo mtaa wa Forest jijini hapa Bwana Said Mohammed amesema elimu itawajenga watoto hao ili wawezesha kuendesha maisha yao kwa njia ya kujitafutia kipato na kutowaacha wakizulula ovyo mtaani na kuachana na dhana tegemezi, kupambana na janga na Ujinga na Umaskini.

Ameyataja maeneo ambayo watoto wengi wamekuwa wakifanyakazi muda ambao walitakiwa wawepo shuleni kuwa ni pamoja na Isanga, Ilemi, Iganzo na Mwanjelwa ambapo watoto hao wamekuwa wakikutwa wakiuza maduka, upondaji kokoto, ufyatuaji na upangaji tofari.

Bwana Said amewataka wazazi kuwapa watoto wao mahitaji muhimu ya mavazi, chakula na malazi ili kuondokana na tatizo hilo.

Post a Comment

 
Top