Menu
 

Marehemu John Mwankenja ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilay ya Rungwe.

Na Mwandishi wetu. 
Diwani wa kata ya Lufilyo Meckson Mwakipungu amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe baada ya mwenyekiti wa awali John Mwankenja kuuawa na majambazi MEI 17 mwaka huu akiwa nyumbani kwake.

Akitangaza matokeo ya nafasi hiyo ya uwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo bwana Noel Mahenga amesema Meckson Mwakipungu ameibuka na ushindi wa kura 40 huku mpinzani wake Anyemike Mwasakilali ambaye ni diwani wa kata ya Kawetere kutoka chama cha NCCR MAGEUZI amepata kura tatu.

Matokea ya uchaguzi huo yamepokelewa kwa furaha na mamia ya wakazi wa wilaya ya Rungwe, huku wakidai kuwa Meckson Mwakipungu anao uwezo mkubwa wa kuleta maendeleo kwenye Halmashauri yao.

Post a Comment

 
Top