Menu
 


 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.
=====
Na mwandishi wetu.
Zaidi ya watu 12 wamepigwa Nondo mpaka sasa kwa muda wa siku 7 ambapo miongoni mwao wakiwemo askari polisi wawili mmoja kutoka kitengo cha usalama barabarani na mwingine katika kitengo cha ufundi Mbeya ambaye alifariki dunia.

Habari za uhakika zinadai kuwa kati ya watu hao 12 watu 11 wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa Mbeya akiwemo askari wa kike kutoka kitengo cha usalama barabarani WP.HAWA ambaye amelazwa katika wodi ya watu mahututi (ICU).

Kutokana na matukio hayo kuanza kuchukuwa kasi kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema kuwa Jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha matukio hayo yanakomeshwa mara moja.

Aidha ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kutoa taarifa za uwepo wa watu wanaodhaniwa kuwa ni wahusika wa matukio hayo ili waweze kudhibitiwa mara moja.

Post a Comment

 
Top