Menu
 

Mamlaka ya maji safi na maji taka jiji la Mbeya imetangaza kutoa zawadi ya shilingi laki tano kwa mtu atakaye toa taarifa ama kufanikisha kupatikana kwa wezi wa vifaa vya kuungia mabomba.

Akiongea na chanzo chetu cha habari cha kuaminika, Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo jijini hapa Injinia SHAURI amesema zawadi hiyo itatolewa ili kudhibiti vitendo vya wizi wa viungio vya mabomba katika mabomba mapya.

Amevitaja vifaa mbavyo vimekuwa vikiibiwa kuwa ni Gate valves zenye kipenyo milimita 75 hadi 400 na kuongeza kuwa mamlaka hiyo itaichukuwa taarifa iliyotolewa kuwa siri kubwa.

Post a Comment

 
Top