Menu
 


Mambo vipi mkuu?,
Barua kwako kuhusiana angalizo la Soko la Ilemi darajani.

Nachotaka kuzungumzia, Jinsi gani pesa inavyotafutwa na wafanyabiashara wadogo wadogo wa bidhaa za chakula ndizi, nyanya, mchele n.k. maeneo ya soko la Ilemi darajani, kuna usemi kila kitu heshima,dharau zote hubebwa zaidi na fedha, ndiyo maana fedha hutafutwa kwa hali na mali,wakati mwingine pesa husakwa kwa njia mbalimbali salama na si halali tena pasipo kujali kuhatarisha maisha kwa lengo la kuwa na maisha bora.

Kaka maeneo ya Ilemi darajani jijini Mbeya nyakati za jioni kuna watu wanafanyabiashara ambao hufanya shughuli hiyo ndani ya barabara ni vema wakaingia ndani kidogo au pembezoni na barabara na walishapewa agizo kuwa waingie ndani au kufanyia biashara mbali kidogo mwa barabara inasemekana waligoma, isitoshe hapo ni mteremko kuna mrundikano mkubwa katika barabara hiyo, na vyombo vya moto/magari kibao, bajaji ndio usiseme, sisi wa baiskel ndio kama sisimizi.

Kama vipi  pita jioni maeneo yetu huone jinsi panavyokua kisha utathmini siku gari ikikosea njia sijui tutaliaje na ajali zitokeazo mara kwa mara mkoani kwetu? Tutapoteza uhai wa watu kibao kimasihala na kama vipi twaomba tuwashauri katika kipindi chako, au kupitia mtandao huu.

Hata hivyo Serikali inapaswa kutilia maanani suala hili kwa lengo la kuepusha maafa.

Naitwa Efratechnology Efrachemical
Toka Ilemi jinini Mbeya
Together we are brother.
"Mdau wa Chimbuko Letu".

Post a Comment

 
Top