Menu
 


Wafanyakazi wakichimba mtaro wa maji
*****
Na mwandishi wetu
Halmashauri ya jiji la Mbeya idara ya miundombinu imeshauriwa kuchimba mifereji pembezoni mwa barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami na zile zilizojengwa kwa kiwango cha udongo ili kusaidia maji kupita kirahisi ili kuzuia mmomonyoko wa udongo barabarani.

Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wafanyabishara wa soko la Mwanjelwa mtaa wa jua kali wakati wa mahojiano na mwandishi wetu kuhusu namna wanavyoweza kukabiliana na maji kutuama pembezoni mwa maduka yao nyakati za mvua.

Mmoja wa wafanyabiashara hao Bwana Vivian Sanga amesema njia pekee itakayosaidia kuondoa maji kutuama kwenye barabara ni kuchimba mitaro pembezoni mwa barabara ili kupitisha maji taka kwa urahisi.

Post a Comment

 
Top