Menu
  *****
Maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yameanza rasmi mkoani mbeya katika viwanja vya shule ya msingi Ruanda Nzovwe ambayo yatafanyika kwa muda wa siku tatu.

Maadhimisho haya yameambatana na maonyesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi kutoka kwa wadau mbalimbali.

Aidha Serikali imeandaa kongamano litakalowajumuisha wadau mbalimbali katika ukumbi wa mkapa uliopo Sokomatola ambapo kupitia kungamano hilo wananachi watajadili mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 50 ya Uhuru.

Post a Comment

 
Top