Menu
 

Madereva wa pikipiki maarufu kama Bodaboda zaidi ya mia nne jijini Mbeya wakiwa katika maandamano baada ya mmoja wao kuuwawa kwa kupingwa nondo.
***** 
Na mwandishi wetu.
Dereva wa pikipiki mkoani Mbeya aliyefahamika kwa jina la Jacob Elias Mwakalobo anayekadiliwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 30 hadi 35, mkazi wa Uyole ameuwawa na mtu au watu wasiofahamika kisha kuporwa pikipiki yake usiku wa kuamkia jana eneo la Uyole jijini Mbeya.

Marehemu Jacob alikuwa akiendesha pikipiki ya kukodishwa maarufu kama bodaboda yenye nambari ya usajili T 676 BRX aina ya T-BETTER yenye rangi nyekundu.

Baba mzazi wa marehemu Bwana Eliud Elias amesema kuwa marehemu aliondoka majira ya saa kumi na moja jioni nakuaga kuwa amekodiwa na abiria na hivyo hakurudi nyumbani kwake hadi mwili wake ulipokutwa katika nguzo za umeme za gridi ya taifa zinazoelekea Sae, huku mwili wake ukiwa na majeraha mbalimbali kichawani. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa madereva hao Bwana Vicent Mwashoma amesikitishwa na tukio hilo kwani mara kwa mara waendesha pikipiki wamekuwa wakiuwawa na kupora pikipiki zao hali inayopelekea wao kufanya kazi kwa hofu.

Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mbeya Anecletus Malindisa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi unafanywa kwa lengo la kubaini wahusika wa mauaji hayo.
 
Mwili wa marehemu Jacob ulichukuliwa kwa maandamano ya zaidi ya pikipiki/bodaboda mia nne kutoka Hospitali ya Rufaa na kuupeleka kuzikwa katika makaburi ya Ilemi jijni Mbeya.

Pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na marehemu na kuporwa ni mali ya Bwana Willy Luambano mwenye umri wa miaka 32 ambaye amesema pikipiki yake ilinunuliwa kwa thamani ya shilimi 1, 425, 000 za kitanzania ambapo marehemu alikuwa akilala nayo na mkataba wa kupeleza mauzo kila wiki.

Post a Comment

 
Top