Menu
 

 Mbunge wa jimbo la Mbarali Mwalimu Kilufi(katikati), akisalimiana na baadhi ya wananchi nje ya mahakama ya Hakimu mfawidhi wa mkoa wa Mbeya.
*****
Na mwandishi wetu.
Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa mkoa wa Mbeya imekamilisha kusikiliza ushahidi wa kesi inayomkabili mbunge wa jimbo la Mbarali Modestus Kilufi na kusema kuwa hukumu ya kesi hiyo itatolewa Novemba 9 mwaka huu.

Hakimu wa mahakama hiyo Michael Mteite amesema baada ya upande wa Serikali na mlalamikaji kutoa ushahidi wao juzi na jana, Mahakama hiyo imekamilisha ushahidi na kilichobakia ni hukumu.

Akitoa ushahidi wake Kilufi amesema kesi inayomkabili hahusiki nayo bali ni njama inayofanywa na baadhi ya viongozi Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Mbarali ili waweze kumondoa madarakani.

Hata hivyo wakili wa Serikali Apimaki Mabrouck alimuuliza swali mbunge huyo kwa nini hakutoa taarifa hizo polisi wakati akiandika maelezo ya awali ambapo mbunge Kilufi alimjibu kuwa asingeweza kutoa maelezo ambayo hakuulizwa.

Mbunge huyo alifikishwa mahakanani hapo Octoba 10 mwaka huu kwa kosa la kumtishia kumuua afisa mtendaji wa kata ya Ruiwa Jordan Masweve machi 16 mwaka huu ambapo kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha sheria 189 cha mabadiliko ya sheria ya mwaka 2002 kifungu kidogo cha 2 (a) sura ya 16 ambapo mshitakiwa alikana shitaka.

Post a Comment

 
Top