Menu
 

Na Furaha Eliab, Chunya
Mfanyakazi wa Kampuni ya utafiti wa madini,
Baflix Limited iliyopo katika wilaya ya Chunya, Sebastian Njile ambaye ni mkazi wa Mkwajuni wilayani hapo amepandishwa kizimbani katika mahakama ya mwanzo Mwambani  iliyopo wilayani humo mkoani Mbeya akikabiliwa na kosa la kumpa mimba binti na kumkataa.

Katika kesi hiyo mshtakia alitakiwa kufika mahanani hapo kujibu mashitaka yanayomkabili mapema siku moja kabla ya tarehe ya kufika mahakani hapo alituma barua mahakamani hapo ya kuomba kuto fika siku ya kesi.

Akitoa maelezo ya awali mahakamani hapo hakimu wa mahakama hiyo Sharif Nyumile alisema mstakiwa wa kesi hiyo Sebastian ameomba kutofika mahakamani hapo kutokana na majukumu ya kikazi ambapo atasafiri nje ya wilaya.

Alisema mshtakiwa huyo amepata safari ya kikazi kuanzia Octoba 4 hadi Octoba 31 mwaka huu ambapo atakuwa amerudi kutoka safari hiyo na kurejea Mkwajuni wilayani hapo.

Aidha hakimu Nyumile alisema kutokana na kutokuwepo kwa mshtakiwa wa kesi hiyo kwa kipindi chote hicho kesi hiyo itasikilizwa tena Disemba 2 Mwaka huu.

Post a Comment

 
Top