Menu
 


Na mwandishi wetu
Mkazi mmoja wa kijiji cha Mpemba wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya John Mpembela mwenye umri wa miaka 55 ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jana usiku

Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Anacletus Malindisa  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea majira saa moja na nusu usiku marehemu akiwa nje ya mlango wa nyumba  yake.

Malindisa amesema marehemu ameuawa kwa kupigwa risasi kwa kutumia bunduki aina ya shortgun ambapo katika mwili wake yamekutwa majeraha mbalimbali ya risasi na maganda yake.

Aidha Kaimu Kamanda amesema chanzo cha kuuwawa Bw. John hakijajulikana na hakuna aliyekamatwa na jeshi la polisi linaendelea na upelelezi . 

Post a Comment

 
Top