Menu
 


Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO amewataka viongozi wa kijiji cha Ikumbi kata ya Bonde la Songwe kuanza kutoa elimu kwa wafugaji wa ng’ombe kijijini hapo kuhusu madhara ya kupitisha mifugo yao kwenye uwanja wa Ndege ili kuondoa hatari zinazoweza kujitokeza hapo baadae.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea uwanja huo wenye urefu wa kilometa 3 nukta 6 na upana wa mita 45 ambapo alikutana na kundi la ng’ombe wakikatisha uwanjani hapo hali inayohatarisha usalama wa anga endapo hatua za haraka hazitochukuliwa mara moja.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho SHIGALA ZAMBI ameahidi kushirikiana na mamlaka ya viwanja vya ndege mkoa kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa uwanja huo katika kuutunza uwanja na kutokatisha uwanjani hapo wao na mifugo yao.

Awali meneja wa kiwanja cha ndege Songwe aliomba msaada kwa Serikali kutoa onyo kwa wakazi wanaoishi pembezoni na uwanja huo kutokatisha uwanjani hapo pamoja na wanakijiji kushiriki kulinda vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa uwanja ili visiibiwe.

Post a Comment

 
Top