Menu
 

Na mwandishi wetu
Mratibu wa shughuli za nje kutoka Kituo cha Utafiti wa Afya mkoa wa Mbeya (MMRP) Bwana Weston Assisya amewataka wanasiasa kutoa ushirikiano kwa kituo hicho ili kuhamasisha jamii kushiriki kwenye tafiti badala ya kupandikiza chuki juu ya tafiti zinazoendelea.

Ameyasema hayo wakati wa mahojiano nasi ofisini kwake juu ya kauli zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa na jamii kuhusu tafiti zinazofanywa na kituo hicho.

Awali baadhi ya viongozi wa kisiasa mkoani Mbeya walikuwa wakitoa lawama kwa Serikali kwa kukubali tafiti za magonjwa mbalimbali kufanywa kwa wananchi kwa madai kupitia tafiti hizo wananchi wamekuwa wakipandikizwa Virusi vinavyosababisha Ukimwi na magonjwa mengine.

Kituo cha Utafiti wa Tiba na Dawa mkoa wa Mbeya (MMRP) kinafanya tafiti za kinga dhidi ya UKIMWI, MARALIA, KIFUA KIKUU, KICHOCHO na MATENDE.

Post a Comment

 
Top