Menu
 

 Toka kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mbeya John Mwakipesile wa pili ni Mstahiki meya wa jiji la Mbeya Mheshimiwa Atanas Kapunga watatu Mzee Ernest Waya wanne ni mwakilishi wa machifu wa Mbeya.
*****
Na mwandishi wetu
Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, kuandaa semina haraka kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo ili kuwaelimisha juu ya kanuni za uendeshaji wa vikao vya Halmashauri.

 Kapunga ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na tamko la CHADEMA, ambalo walilitoa wakimtaka ajiuzulu wadhifa wake.

 Aidha agizo hilo la Meya limekuja ikiwa ni siku mbili baada ya  madiwani CHADEMA,  kususia kikao cha Baraza la Madiwani, kitendo ambacho KAPUNGA anaamini kimechangiwa na madiwani hao kutokuzijua kanuni na sheria za uendashaji wa vikao vya Baraza la Halmashauri.

Post a Comment

 
Top