Menu
 

Kamanda wa Jeshila Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi
*****
Na mwandishi wetu
Bwana John Mwakilembe mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa Isanga jijini Mbeya amefikwa na mauti baada ya kung'atwa na nyuki, Oktoba 16, mwaka huu majira ya saa saba mchana na wengine wawili kujeruhiwa.

Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa mtaa wa Ilolo kata ya Isanga jijini Mbeya Bwana Anjelo Sanga amewataja waliojeruhiwa na nyuki hao na kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya  kuwa ni pamoja na Bwana Mboka Masapa na Meblon Mofat.

Taarifa za kundi hilo la nyuki lilitolewa na Bwana Felix Mkusa ambaye alimtaarifu balozi wa shina hilo Bwana Lukomano Mwakatobe ambaye aliita wananchi kumsaidia marehemu baada ya kundi la nyuki kupamba kichwani mwake.

Marehemu amefikwa na tukio hilo wakati akiwa katika shughuli zake binafsi za uuzaji wanyama ndipo kundi hilo la nyuki lilipofika na kumshambulia hadi mauti yalivyomfika ambapo wasamalia wema waliokuwa wakijaribu kuokoa maisha yake walikuwa wakiwakimbiza na kisha kurudi tena kwa marehemu.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kifo, katika maeneo ya Bar ya Omega iliyopo kata ya Isanga jijini Mbeya.

Post a Comment

 
Top