Menu
 

Kamanda wa Jeshila Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi
*****
Na mwandishi wetu
Dereva wa gari aina ya Scania lenye namba za usajili T.646 ARA, Bwana Husein Ibrahimu mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Mbozi mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya tairi la mbele la gari hilo la upande wa kulia kupasuka kisha gari kupinduka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Mbimba wilaya ya Mbozi ambapo dereva wa gari hilo alifariki dunia papo hapo.

Ameongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni tairi la Mbele kupasuka na mwendo kasi.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Vwawa Mbozi na gari hilo lipo katika kituo cha Polisi Vwawa.

Post a Comment

 
Top