Menu
 

 Ofisi ya Afisa mtendaji wa Kata ya Isanga jijini Mbeya ikiwa imefunguliwa na kuachwa wazi pasipo kuwepo na mtu yeyote kwa zaidi ya masaa matatu, kuanzia muda wa majira ya saa 5 asubuhi hadi saa 8 mchana ikiwa mida ambayo mtumishi anatakiwa kuwa kazini kutatua matatizo ya jamii, halikadharika nyaraka za serikali zikiachwa. Je huu ni Uwajibikaji kwa watendaji wa serikali, hivi Maadili ya viongozi na utawala bora yanazingatiwa.
Mtandao huu umeweza kumsubiri Afisa Mtendaji wa Kata ya Isanga jijini Mbeya Bi Ever George kwa takribani muda wa masaa matatukuanzia muda wa majira ya saa 5 asubuhi hadi saa 8 mchana, na hakuwa tayari kupokea simu yake, Je wangapi wanapata usumbufu katika kata zetu, Sekretarieti ya Maadili ya viongozi na Utawala bora inapaswa kuchunguza tabia hizi kwa mtu aliyepewa dhamana ya kuitatulia matatizo jamii.

Post a Comment

 
Top