Menu
 


 Na mwandishi wetu
Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya imebainika kuwa na kasoro kadhaa katika taarifa ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2009/2010 licha ya kupata hati safi katika mwaka huo.

Kasoro hizo za mapungufu katika utendaji zinatokana na taarifa ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG zilizobainishwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kwenye kikao cha baralaza maalumu la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika kwa ajili ya kupitia taarifa hiyo.

 Akifungua kikao hicho mkuu wa mkoa Kandoro, amesema pamoja na halmashauri ya Ileje kupata hati safi yapo maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa ujumla na kuwekewa msisitizo ili kuongeza ufanisi.

Ameyataja maapungufu hayo kuwa ni kuhamisha fedha toka akaunti ya maendeleo kwenda akaunti za matumizi ya kawaida za zaidi ya shilingi milioni 99 na laki 9 na zaidi ya shilingi milioni 78 laki 8.

Akijibu hoja hizo mkurugenzi wa halmashauri hiyo Glads Dyamvunye amesema baadhi ya kasoro zilizobainishwa kwenye taarifa hiyo tayari zimeafanyiwa kazi ikiwemo kurejeshwa kwa kiasi fedha za miradi zilizohamishwa kwenye akaunti yake.

Post a Comment

 
Top