Menu
 


Mkuu Mpya wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro baada ya kumaliza kula kiapo sasa aanza kuutumikia Mkoa wa Mbeya.
*****
Na mwandishi wetu
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka madiwani na watendaji katika halmashauri za wilaya kila mmoja kutambua, kuthamini na kuwajibika ipasavyo katika shughuli za kiutendaji ndani ya jamii.

Bwana Kandoro ameyasema hayo hivi karibuni katika kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ileje kilicholenga kujadili taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali CAG.

Amesema wapo baadhi ya madiwani na watendaji ambao wamekuwa wakiyasahau majukumu yao na kujikuta wanaendekeza siasa katika kila wanalofanya pasipo kutambua kuwa kufanya hivyo kunawacheleweshea maendeleo wananchi katika maeneo yao.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Glads Dyamvunye alisema ukosefu wa vyanzo vya mapato ni changamoto kubwa kwa halmashauri yake hali inayopelekea kuendelea kuwa tegemezi kwa serikali kuu.

Post a Comment

 
Top