Menu
 

Hawa ni waandishi  wa habari mkoani mbeya kwa miaka minne iliyopita wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano wa MKAPA uliopo jijini Mbeya na kupiga picha ya pamoja.
*****
Na mwandishi wetu
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amefanya ziara maalumu ya kutembelea ofisi ya Chama Cha waandishi wa habari mkoani hapa na kusisitiza ushirikiano wa kutoa na kupata taarifa kutoka Serikalini.

Aidha amewataka wakuu wa idara wa halmashauri na Serikali kuhakikisha wanatoa taarifa kwa waandishi wa habari ili kuiwezesha jamii kufahamu mambo muhimu yanayoendelea mkoani mwao.

Kuhusu suala la Pembejeo Kandoro amesema pembejeo hizo za Ruzuku zimeanza kusambazwa kwa wilaya ya Mbeya na Rungwe huku akitoa onyo kali kwa mawakala ambao hawatatekeleza maagizo yaliyotolewa na Serikali katika ugawaji wa pembejeo hizo.

Kwa upande wa masoko amesema ofisi yake imeandaa kamati ya kukabiliana na majanga ya moto ambapo kamati hiyo itakuwa na jukumu la kupanga miundombinu ya Soko ili kurahisisha zoezi la ukoaji kufanyika kiurahisi pindi moto unapotokea.

Wakati huohuo ameitaka jamii kushiriki kikamilifu katika ulinzi pamoja na kufanya kazi kwa bidii badala ya kutumia njia za mkato kujipatia kipato kwa imani za kishirikina.

Post a Comment

 
Top