Menu
 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka kumjulia hali mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mh. Zitto Kabwe juu ya hatua ya ofisi ya bunge kumsafirisha nchini India kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akiongozwa na daktari wa magonjwa dharura Dk. Juma Mfinaga (kulia) wakati alipofika katika hospitali ya Taifa Muhimbili kumjulia hali Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mh. Zitto Kabwe.
Baadhi ya watu waliofika kumjulia hali mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe wakiwa nje ya chumba cha Min ICU alikolazwa mbunge huyo wakati walipofika kumjulia hali.
Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulila akibadilishana mawazo na mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (kati) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda (shoto) wakati walipofika kumjulia hali mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe jioni hii katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akisalimiana na madaktari wakati alipowasili katika hospitali ya Taifa ya muhimbili jioni hii kumjulia hali mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto kabwe.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akimjulia hali mbunge wa viti maalumu Masasi, Clara Mwituka wa CUF ambaye amelazwa jana katika hospitali ya Taifa Muhimbili akisumbuliwa na Vidonda vya tumbo pamoja na Presha. Kulia ni Daktari wa magonjwa ya dharura, Dk. Juma Mfinanga na Professa Victor Mwafongo ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Magonjwa ya dharura.

Na Francis Dande

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Anne Makinda jioni hii amefika katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili na kumjulia hali Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye amelazwa katika chumba cha Min ICU.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, Spika Makinda alisema kuwa ofisi yake inaandaa utaratibu wa kumpeleka Mh. Zitto nchini India ili akapate matibabu zaidi.

‘Hali ya mgonjwa sio mbaya lakini tutaandaa utaratibu wa kumsafirisha kwenda India pindi madaktari watakapomuandaa mgonjwa tayari kwa safari hiyo na taarifa tutazitoa ni lini hasa atasafirishwa alisema Mh. Spika’.

Naye Professa Victor Mwafongo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Kitengo cha Magonjwa ya dharura pamoja na Dk. Juma Mfinanga ambao ndio wanaomshughulikia mgonjwa huyo walisema kuwa mgonjwa huyo hali yake sio mbaya sana ila anahitaji muda mwingi wa kupumzika kitu ambacho kwa sasa kinakosekana kutokana na idadi kubwa ya ndugu jamaa na marafiki kufika hospitali hapo kutaka kumjulia hali.

Aidha Dk. Juma Mfinanga aliongeza kuwa taarifa zaidi kuhusu hali ya Mh. Zitto ikiwemo safari ya kupelekwa India itatolewa pindi itakapokuwa tayari.

Post a Comment

 
Top