Menu
 

 Sio kuwatenga, sio kuwaacha kwani sote ni ndugu wapewe haki zao kwani hawakujitakiwa kuwa walemavu.
+++++
Na mwandishi wetu.
Serikali, makampuni wa wadau mbalimbali wa masuala ya ujenzi nchini wametakiwa kujenga majengo kwa kuzingatia kuweka miundombinu sahihi ambayo itawawezesha walemavu kupata haki zao za kimsingi au huduma halali katika majengo hayo.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu mwenyekitio wa Chama cha walemavu Tanzania ndani ya mkoa wa Mbeya (CHAWATA) Bwana Jimmy Ambilikile wakati wa mahojiano na chanzo hiki.

Amesema iwapo majengo ya huduma muhimu yatajengwa kwa kuzingatia mazingira ya kundi hilo maalumu yatawezesha malemavu kupata huduma zao bila usumbufu wa aina yoyote.

Walemavu wamekuwa wakishindwa kufikia huduma muhimu za kijamii kutokana na makandarasi wa ujenzi kutojenga majengo yao kwa kutokufikilia kundi hilo maalumu.

Aidha uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa ofisi mbalimbali zikiwemo taasisi za kifedha, afya na vyuo kutokuwa na miundombinu bora inayowawezrsha walemavu kupata huduma zao kwa urahisi.

Post a Comment

 
Top