Menu
 


Serikali angalieni hili ili kutimiza Azima kuimalisha Sekta ya Elimu kwa lengo la kufuta Ujinga kwani watoto wanahitaji kupata Elimu bora sawa na wengine na hakuna lisilowezekana, kwani sehemu nyingine mmeweza kutekeleza uboreshaji wa Miundombinu. Haki sawa daima ili watoto wapate kusoma na kuandika kwa ufasaha.
*****
Na mwandishi wetu
Wanafunzi wa shule ya msingi ilolo iliyopo kata ya Isanga jijini Mbeya wanasoma katika mazingira magumu kutoka na madarasa ya shule hiyo kutosakafiwa kwa kutumia saruji.

Pia madarasa ya shule hiyo hayana madirisha hali inayowawia vigumu watoto kuelewa wanayofundishwa na walimu wao kutokana na baridi pamoja na vumbi inayoingia darasani kipindi cha kiangazi.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Filemon Mbepela amesema ukosefu wa fedha ni sababu kubwa iliyopelekea madarasa hayo kutosakafiwa kwa kutumia saruji ambapo wananchi wa kata ya Isanga wameshindwa kuchangia fedha ili kuwasaidia watoto wao kusoma katika mazingira bora.

Ameongeza kuwa shule hiyo pia inakabiliwa na ubovu wa Vyoo,  uchache wa waalimu na kutokuwa na wigo hali inawawia vigumu waalimu kudhibiti tatizo la utoro kwa wanafunzi.

Aidha ameiomba jamii na Serikali kuchangia vitu mbalimbali vitakavyosaidia kukamilisha ukarabati wa madarasa ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.

Post a Comment

 
Top