Menu
 

 Na mwandishi wetu.
Wakazi wa jiji la Mbeya wameshauriwa kupanda miti katika mazingira yanayozunguka nyumba zao ili kuzuia mmomonyoko hasa katika kipindi cha masika ikiwa ni pamoja na kupendezesha mazingira ya jiji.

Ushauri huo umetolewa na mmiliki wa bustani ya matunda na kivuti eneo la mafiati kata ya Iyela jijini hapa Bi. Bahati Kyomo.

Amesema miti inafaida kubwa katika maisha ya binadamu ikiwa ni kupunguza joto, mazingira kuvutia na hewa safi ya Oksijeni ambayo imekuwa ikiharibiwa na hewa chafu kutoka viwandani.

Wakati huohuo ameiomba halmashauri ya jiji la Mbeya kutoa semina na matangazo ya barabarani yanayohamasisha watu kupanda miti ili kurejesha hali nzuri ya kewa jijini hapa ambayo ipo hatarini kutoweka kutokana na uharibifu wa mazingira utokanano ya moshi wa kemikali toka viwandani.

Post a Comment

 
Top