Menu
 

Prof Mark Mwandosya.

Prof Mark Mwandosya ambaye ni Waziri wa maji na Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki.
*****
Na mwandishi wetu
Wananchi wa Jimbo la Rungwe Mashariki wamefanya ibada maalum ya kumwombea Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni  Waziri wa maji Profesa. Mark Mwandosya ili apone haraka.

Baada ya ibada hiyo maalumu mmoja wa wakazi wa jimbo hilo Njwaba Mwakambinda amesema wananchi wa Kijiji hicho wanafarijika wanaposikia taarifa njema kuhusu hali ya afya ya Mbunge wao.

Naye mwenyekiti wa wataalamu mkoa wa Mbeya Prince Mwaihojo amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuondoa itikadi zao za kisiasa katika kuleta maendeleo katika Jimbo hilo na kuombeana mema badala ya kutumia siasa kuzushiana vifo.

Akijibu baadhi ya masuala yaliyojitokeza eneo hilo, Msaidizi wa Prof. Mark Mwandosya, Ndigwako Mwasandungila ambaye pia ni diwani wa kata ya Lwangwa amesema mbunge wao anaendelea vizuri na anaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi zake akiwa kwenye matibabu.

Post a Comment

 
Top