Menu
 

Na mwandishi wetu
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Maanga Bwana Lusajo Mwakaje amesema kuwa watoto yatima wanaosoma kwenye shule hiyo wanakabiliwa na tatizo la vifaa vya shule pamoja na sare za shule.

Akiongea na Mwandishi wetu ofisi kwake bwana Mwakaje amesema wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu wa kusimamia usafi kwa wanafunzi kutoka na wanafunzi hao kudai kuwa hawana sare za shule na fedha kwa ajili ya kupeleka sare hizo kwa fundi pindi zinapochanika.

Aidha ameiomba jamii kujitolea kuwapatia huduma muhimu watoto yatima wanasoma shuleni hapo ambao hawana wafadhili wa kuwapatia huduma muhimu za msingi.

Post a Comment

 
Top