Menu
 

Kamanda wa Jeshila Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi
*****
Na mwandishi wetu
Watu wawili wamefariki dunia papo hapo katika matukio ya ajali za barabarani yaliyotokea jana kwenye maeneo mawili tofauti mkoani Mbeya.

Akiongelea matukio hayo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema tukio la kwanza limetokea wilayani Chunya barabara ya makongorosi ambapo mtoto Rajabu Yasini mwenye umri wa miaka 2 aligongwa na gari aina ya benzi lenye namba za usajili T.866 ACD lililokuwa likiendeshwa na Haruna Halfani mwenye umri wa miaka 48 na kufariki dunia papo hapo.

Tukio la pili limetokea wilaya mpya ya Momba katika maporomoko ya Tunduma ambapo basi la Abood lenye namba za usajili T.297 ATH lililokuwa likiendeshwa na Brown Masako mwenye umri wa miaka 43 lilimgonga Amani Chengula msukuma mkokoteni mwenye umri wa miaka 32 na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kutokana na matukio hayo madereva wote wawili wamekamatwa na magari yao yapo kwenye vituo vya polisi ambapo vyanzo vya ajali hizo ni mwendo kasi.

Aidha kamanda NYOMBI amesema kuwa watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Post a Comment

 
Top