Menu
 

 Na mwandishi wetu.
Wazazi wametakiwa kujenga ushirikiano na walimu kwa kufuatilia mwenendo wa maendeleo ya elimu kwa watoto wao ili kudhibiti nidhamu na utoro mashuleni.

Hayo yamesemwa na mkuu wa shule ya Southern Highland Mbeya Mwalimu Chamila Evarist wakati wa mahojiano na mwandishi wetu kuhusu sababu inayochangia wanafunzi kufanya vibaya kwenye mitihani yao.

Amesema njia pekee ya kuwaokoa wanafunzi katika wimbi la kufeli mitihani yao ni wazazi kufuatilia mwenendo wa kimasomo kwa watoto wao ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kukagua mara kwa mara madaftari ya watoto wao.

Post a Comment

 
Top