Menu
 


Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu
(katikati).
*****
Na mwandishi wetu.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji  na uwezeshaji Dkt.Mary Nagu (Mb) amezitaka taasisi na vyombo vya dola kuweka mazingira wezeshi  ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa wawekezaji katika Tanzania  ili kusiwepo na vikwazo na ucheleweshwaji wa huduma muhimu.

 Dkt. Nagu aliyasema hayo  jana wakati wa ufunguzi wa kituo cha uwekezaji kwa kanda ya  nyanda za juu kusini kilicho ofisi za Bank ya NBC Jijini hapa.

Alisema kuwa  ili wawekezaji  wa kanda ya Mbeya waweze kufanya kazi vizuri hakuna budi vikwazo vyote kuondolewa na upatikanaji wa huduma muhimu kwa wawekezaji urahisishwe. Hata hivyo waziri Nagu alihimiza mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kutenga, kupima na kusajili maeneo ya uwekezaji ipasavyo kabla ya kuyagawa pale inapowezekana ili kuondoa usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

 Alisema ikumbukwe kuwa uwekezaji  ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa nchi  kwani  utaongeza pato la Taifa, mitaji na teknolojia na ajira kwa watanzania wengi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kituo cha Uwekezaji cha Tanzania Balozi Elly Mtango alisema kituo hicho kinategemea  kufanya kazi  na mamlaka nyingine za mikoa na serikali za mitaa na vijiji katika kufanikisha upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya shughuli za uwekezaji na uendelezaji wa miuondo mbinu.

 Aidha alitoa wito kwa wafanyabishara na wawekezaji wote katika kanda ya mbeya  kutumia kituo hicho katika kujipatia huduma mbali mbali ili wajiendeleze kibiashara na kiuwekezaji.

Post a Comment

 
Top