Menu
 


Na mwandishi wetu
Halmashauri ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imetumia zaidi ya shilingi milioni mia moja sitini na mbili katika ukarabati wa zahanati saba ambazo ni Makwale, Itope, Busale, Ngonga, Bujonde, Lugombo na Njisi wilayani humo.

Fedha hizo zimetolewa na Serikali kuu ni kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) katika kipindi cha mwaka 2008/2010.
  
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bwana Mhando Senyagwa amesema fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi mingine iliyotekelezwa kwa kukarabati kituo cha Afya cha Ipinda na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo pamoja na ukarabati wa Zahanati za Katumbasongwe, Ipande na Njugilo ambazo tayari zimekamilika.

Post a Comment

 
Top