Menu
 

Jeshi la polisi mkoani Mbeya limefanikiwa kukamata gari iliyoibiwa kitongoji cha Ichenjezya wilayani Mbozi yenye nambari za usajili T 669 DCK aina ya Toyota Prado inayomilikiwa na Kampuni ya Bablo yenye makao makuu wilayani humo mkoani humo na kukamatwa jijini Mbeya.

Gari hiyo iliibiwa majira ya saa tano asubuhi Novemba 23, mwaka huu, nyumbani kwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo ambapo ndani ya gari kulikuwa na watoto wawili ambao walitelekezwa njiani.

Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la ujambazi na kwama watu wawili wanashikiliwa na Jeshi hilo la polisi.

 Hata hivyo imedaiwa kuwa hilo ni tukio la pili kutokea ambapo la kwanza lilitokea Novemba 21, mwaka huu wilayani Mbozi ambalo nalo lilikamatwa eneo la Mlowo wilayani humo.

Post a Comment

 
Top