Menu
 

Na mwandishi wetu
Bariki Sanga mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Uyole jijini Mbeya ambaye alikuwa akifanya biashara ya ulanguzi wa mpunga katika kijiji cha Wimba mahango kata ya Igurusi amekutwa akiwa amefariki dunia ndani ya shimo la Choo huku mwili wake ukiwa umeharibika vibaya.

Mwili wake umekutwa ndani ya choo ukiwa umewekwa kwenye gunia na kufungwa na nguo mbalimbali jana majira ya saa kumi za jioni baada ya ndugu na marafiki kumtafuta kwa zaidi ya wiki moja.

Kutokana na tukio hilo mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Witson Kazimoto amewataka wananchi wa kijiji hicho washirikiane na Jeshi la polisi ili kuweza kumpata Bariki Mbariko ambaye anadaiwa kuwa mara ya mwisho alikuwa na marehemu na walikuwa wamekubaliana kwenda kulangua mpunga.

Inadaiwa kuwa marehemu huyo alikuwa na fedha taslimu shilingi laki sita na alizikwa jana usiku jirani na eneo alilokutwa kutokana na mwili wake kuharibika vibaya hivyo kushindikana kusafirishwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa hadi sasa Jeshi la polisi linawashikiria watu wawili kwa kuhusika na tukio hilo.

Post a Comment

 
Top