Menu
 

 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.
*****
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mtu mmoja amefariki dunia mkoani Mbeya baada ya kugongwa na gari aina ya Scania barabara ya Mbeya/Tukuyu majira ya saa tisa alasiri.

Marehemu amefahamika kwa jina la Bi Renata Kanywani (50) mkazi wa Ndaga wilaya ya Rungwe ambapo aligongwa alipokuwa anatembea kwa miguu na kufariki papo hapo.

Marehemu Renata aligongwa na gari lenye nambari za usajiri T 759 BDD aina ya Scania likiwa na tela lenye nambari za usajili T 456 BDA lililokuwa likiendeshwa na dereva Bwana SamwelMahinya (40) mkazi wa Mama John jijini Mbeya.

Dereva alikimbia kusikojulikana na kulitelekeza gari eneo la tukio.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Makandana wilaya ya Rungwe na gari kufikishwa katika kituo cha Polisi Tukuyu wilayani humo.

Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Post a Comment

 
Top