Menu
 

Na mwandishi wetu
Mtoto Atanasi Aloni mwenye umri wa miaka 13 na mwanafunzi wa shule wa darasa la nne shule ya msingi Msongwi amefariki dunia baada ya kunaswa na umeme akiwa kwenye harakati ya kukata matawi ya miti iliyokuwa jirani na nyaya za umeme.

Tukio hilo limetokea leo hii majira ya saa 3 kamili za asubuhi ambapo mtoto huyo akiwa na kaka yake Ezekiel alifikwa na mauti baada ya tawi alilokuwa analikata kundondokea kwenye umeme wa gridi ya Taifa eneo la Pipe line kata ya Mwakibete jijini hapa.

Habari zaidi zinadai kuwa kabla ya mtoto huyo kufikwa na mauti alikuwa na mama yake mzazi shambani wakipanda mahindi na muda mfupi ndipo kaka yake limwita na kumuomba mdogo wake apande juu ya mti kwa ajili ya kukata matawi kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo Bi.Tabu Mwakalenga.

Aidha kuhusu tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema kuwa hajafikishwa taarifa na kuahidi kuzitolea ufafanuzi baada ya kumfikia ofisini kwake.

Post a Comment

 
Top