Menu
 

Na mwandishi wetu.
Jeshi la polisi linawashikilia raia 9 wa kisomali kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria ambapo kati yao mmoja ndiye aliyetambulika kwa jina la Noa Abdala mwenye umri wa miaka 18.

Akiongelea kukamatwa kwa rai ha wa kigeni kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anacletusi Malindisa amesema watuhumiwa hao wamekamtwa jana eneo la Ilongo wilayani Mbarali mkoani Mbeya ambapo inadaiwa watuhumiwa walikuwa wakiishi eneo hilo kwa muda mrefu.

Ameongeza kuwa watuhumiwa wote 9 wamekamatwa na wamewekwa mahabusu kwa ajili ya mahojiano zaidi na kwamba watafikishwa mahakamani mara baada ya mahojiano kukamilika.

Post a Comment

 
Top