Menu
 


HOSPITALI YA MBOZI MISSION KAMA INAVYOONEKANA.
Na mwandishi wetu
Kampuni ya Lima Ltd ambayo inajishughulisha na ununuzi wa zao la Kahawa nchini imetoa mchango wa fedha taslim Shilingi Millioni ishirini (20,000,000) kwa ajili ya kukarabati jengo la wodi ya wazazi katika hospital ya wilaya ya Mbozi, Mbozi mission iliyopo mkoani Mbeya.

Akikabidhi msaada huo, Meneja wa kampuni hiyo Tinson Nzunda alisema kuwa kampuni yake imeamua kufanya hivyo kwa kuona umuhimu wa hospitali hiyo kwa jamii nzima ya wilaya ya Mbozi.

Nzunda alisema kampuni yake licha ya kutoa msaada huo lakini itaendelea kufanya hivyo katika taasisi mbalimbali za kiserikali na za binafsi zinazojihusisha na masuala ya kijamii.

Kwa upande wake Mganga mkuuu wa Hospitali hiyo Ezekiel Mkoma alishukuru kupata msaada huo wa fedha na kwamba uongozi wa Hospitali hiyo ulipopata fedha hizo tayari zimesha tumika kwa kazi iliyokuwa imepangwa ya kukarabati wadi ya wazazi ambayo ilikuwa imechakaa kwa muda mrefu.

Mkoma aliwataka wadau wa kahawa  wilayani humo, kuiga mfano wa kampuni hiyo ya Lima ambayo inajishughulisha na biashara ya ununuzi wa kahawa wilayani humo kwa kutoa mchango katika taasisi mbalimbali zinazo husiana na jamii kwa ukaribu zaidi ili kurejesha faida kwa wadau.

Aidha Mkoma aliendelea kueleza kuwa hospitali yake inaupungufu wa vifaa vya utafiti wa magonjwa ya zinaa pamoja na ukimwi ingawa ina uwezo wa kuhudumia zaidi ya wakazi Laki tatu ambao baadhi yao ni kutoka katika wilaya za jirani za Ileje na Chunya

Akiongea kwa niaba ya akina mama wajawazito Salima Mwampashe alisema kuwa anaishukuru  kampuni ya Lima kwa kutambua umuhim wa wajawazito wilayani humo.

Post a Comment

 
Top