Menu
 

Bwana Nasib Edson Mwamloka mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Malamba wilaya ya Mbarali, ambaye anasambaza umeme, unaozalishwa mashine ya Power Tiller. Ambapo ametumia injini ya Powertiller pamoja na Mota kama inavyoonekana katika picha ambavyo vinathamani ya shilingi milioni Moja la laki nane za kitanzania.
Baada ya kuzalisha umeme uliobuniwa na Bwana  Nasib Edson Mwamloka husambaza umeme huo katika katika kijiji hicho ambapo mpaka sasa jumla ya Kaya 20 hunufaika na kila kaya hulazimika kulipia shilingi mia Sita kwa siku. 

Bwana Nasib hupata faida ya shilingi elfu ishirini kila siku, na utalamu huo alijifunza katika Chuo cha Ufundi kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki jijini Mbeya mwaka 2000. Ubunifu huo ameweza kujikomboa kiuchumi ambapo mpaka sasa anamiliki nyumba ya kuishi, pikipiki na mashine ya kusaga nafaka.

Post a Comment

 
Top